Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 69

Al-An'aam 6:69

الأنعام

وَمَا عَلَى ٱلَّذِينَ يَتَّقُونَ مِنْ حِسَابِهِم مِّن شَىْءٍ وَلَـٰكِن ذِكْرَىٰ لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ

Maana

Wala hakuna jukumu lolote kwa wale wamchao Mungu, lakini ni kukumbusha tu, asaa wapate kumcha Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala wamchao Mungu hawana jukumu lolote kwao, lakini ni kukumbusha, asaa wapate kujiepusha. [69]

[69] Na wenye kumcha Mwenyezi Mungu hawana dhambi katika dhambi za hawa madhaalimu, ikiwa wataendelea na upotovu wao. Lakini yapasa kuwasemeza na kuwakumbusha, asaa huenda wakaiogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu, na wakaacha upotovu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale Waumini wanaomuogopa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, wakatii amri Zake na wakaepuka makatazo Yake, hawana jukumu lolote juu ya hesabu ya Allah Mtukufu kwa wale wenye kuzama kwenye maneno yasiyofaa, wenye kuzifanyia shere aya za Allah Mtukufu. Lakini ni juu yao wawaidhie waache kuleta maneno hayo ya batili, ili wamche Allah Mtukufu, Aliyetukuka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net