Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 68

Al-An'aam 6:68

الأنعام

وَإِذَا رَأَيْتَ ٱلَّذِينَ يَخُوضُونَ فِىٓ ءَايَـٰتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا۟ فِى حَدِيثٍ غَيْرِهِۦ ۚ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ ٱلشَّيْطَـٰنُ فَلَا تَقْعُدْ بَعْدَ ٱلذِّكْرَىٰ مَعَ ٱلْقَوْمِ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Maana

Na unapowaona wanaoziingilia Aya zetu, basi jitenge nao mpaka waingilie mazungumzo mengine. Na kama Shetani atakusahaulisha, basi baada ya kutanabahi usikae pamoja na watu madhalimu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na unapo waona wanao ziingilia Aya zetu, basi jitenge nao mpaka waingilie mazungumzo mengine. Na kama Shet'ani akikusahaulisha, basi baada ya kutanabahi usikae pamoja na watu madhaalimu. [68]

[68] Na ukihudhuria katika baraza za makafiri, ukawakuta wanazikosoa Aya za Qur'ani, au wanazifanyia maskhara, basi wewe waepuke mpaka watapo ingia katika mazungumzo mengine. Na ukisahau na ukakaa nao wakati wa mazungumzo yao hayo mapotovu, kisha ukaikumbuka amri ya Mwenyezi Mungu ya kujitenga nao, basi usikae tena na watu madhaalimu baada ya kukumbuka.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na uwaonapo, ewe Mtume, washirikina wanaoleta maneno juu ya aya za Qur’ani, kwa urongo na kwa kufanya shere, jiepushe na wao mpaka waingie kwenye maneno mengine. Na iwapo Shetani amekusahaulisha jambo hili, basi baada ya kukumbuka usikae pamoja na watu wenye uadui walioleta maneno ya urongo juu ya aya za Allah Mtukufu,

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net