Al-An'aam 6:83
الأنعاموَتِلْكَ حُجَّتُنَآ ءَاتَيْنَـٰهَآ إِبْرَٰهِيمَ عَلَىٰ قَوْمِهِۦ ۚ نَرْفَعُ دَرَجَـٰتٍ مَّن نَّشَآءُ ۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ
Na hizo ndizo hoja zetu tulizompa Ibrahim dhidi ya kaumu yake. Tunamnyanyua tumtakaye daraja mbalimbali. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye hekima, Mwenye kujua yote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hizo ndizo hoja zetu tulizo mpa Ibrahim kuhojiana na watu wake. Tunamnyanyua kwa vyeo tumtakaye. Hakika Mola Mlezi wako ni Mwenye hikima na Mwenye ujuzi. [83]
[83] Na hiyo hoja kubwa ya Ungu wetu, na Umoja wetu, tulimpa Ibrahim aisimamishe kupambana na watu wake, naye kwa hiyo akatukuka juu yao. Na mtindo wetu kwa waja wetu ni kuwa tunamnyanyua madaraja kwa ujuzi na hikima tumpendaye katika wao. Hakika Mola Mlezi wako, ewe Nabii, ni Mwenye hikima. Huweka kila kitu pahala pake. Ni Mwenye kuwajua wepi wanastahiki kutukuzwa, na wepi hawastahiki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hoja hiyo ambayo Ibrãhîm, amani imshukie, aliwahoji nayo watu wake ndiyo hoja yetu tuliyomuongoza nayo mpaka hoja yao ikakatika. Tunamnyanyua daraja tunayemtaka, miongoni mwa waja wetu, ulimwenguni na Akhera, Hakika Mola wako ni Mwenye hekima katika kuendesha mambo ya waja Wake, ni Mjuzi kuhusu wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net