Al-An'aam 6:84
الأنعاموَوَهَبْنَا لَهُۥٓ إِسْحَـٰقَ وَيَعْقُوبَ ۚ كُلًّا هَدَيْنَا ۚ وَنُوحًا هَدَيْنَا مِن قَبْلُ ۖ وَمِن ذُرِّيَّتِهِۦ دَاوُۥدَ وَسُلَيْمَـٰنَ وَأَيُّوبَ وَيُوسُفَ وَمُوسَىٰ وَهَـٰرُونَ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ
Na tukamtunuku (Ibrahim) Is-haq na Yaakub. Kila mmoja wao tulimwongoa. Na Nuhu tulimwongoa kabla. Na katika kizazi chake tulimwongoa Daud na Suleiman na Ayyub na Yusuf na Musa na Harun. Na hivi ndivyo tunavyowalipa wafanyao mazuri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tukamtunukia (Ibrahim) Is-haq na Yaakub. Kila mmoja wao tulimwongoa. Na Nuhu tulimwongoa kabla. Na katika kizazi chake tulimwongoa Daud na Suleiman na Ayyub na Yusuf na Musa na Harun. Na hivi ndivyo tunavyo walipa wafanyao wema. [84]
[84] Na Sisi tulimpa Ibrahim, Is-haq na Yaaqub bin Is-haq. Na tukamwezesha kila mmoja wao kufikia Haki na Kheri, kama baba yao. Na kabla yake tulimwezesha Nuhu hivyo hivyo, na tukawaongoa katika wazao wa Nuhu, Daud, na Suleiman, na Ayyub, na Yusuf, na Musa, na Harun. Kama tulivyo walipa hawa, tunawalipa wafanyao wema kwa wanavyo stahiki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tulimneemesha Ibrãhîm, amani imshukiye, kwa kumruzuku Isḥãq kuwa mtoto wake na Ya‘qûb kuwa mjukuu. Na wote wawili tuliwaongoza kwenye njia ya uongofu. Pia tulimuongoza Nûḥ kwenye haki, kabla ya Ibrãhîm na Isḥãq na Ya‛qûb. Na pia tuliwaongoza kwenye haki, kati ya kizazi cha Nûḥ, Dãwûd, Sulaimãn, Ayyûb, Yûsuf, Mûsã na Hãrûn, amani iwashukie. Na kama tulivyowalipa Manabii hawa kwa wema wao, ndivyo tunavyomlipa kila mwema.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net