Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-An'aam
Sura ya 6

Al-An'aam

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 82

ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَلَمْ يَلْبِسُوٓا۟ إِيمَـٰنَهُم بِظُلْمٍ أُو۟لَـٰٓئِكَ لَهُمُ ٱلْأَمْنُ وَهُم مُّهْتَدُونَ 82

{82} Yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema kwa kutoa hukumu kati ya makundi haya mawili: "Wale ambao waliamini, na hawakuchanganya imani yao na dhuluma, hao ndio wana amani, na wao ndio walioongoka." Amani kutokana na yenye kuhofisha, na adhabu, na mashaka, na uwongofu kwenda katika njia iliyonyooka. Na ikiwa hawakuichanganya imani yao na dhuluma hata kidogo, si kwa ushirikina wala kwa maasia, basi wangepata amani kamili na uwongofu kamili. Na ikiwa hawakuichanganya imani yao na ushirikina peke yake, lakini wanafanya mabaya, basi wanapata msingi wa uwongofu na msingi wa amani, hata kama hawakufikia ukamilifu wake. Maana ya Aya tukufu isiyokuwa ya moja kwa moja ni kwamba wale ambao hawakupata mambo yote mawili, ni kwamba hawakupata uongofu wala amani, bali fungu lao ni upotofu na mashaka.