Al-An'aam 6:8
الأنعاموَقَالُوا۟ لَوْلَآ أُنزِلَ عَلَيْهِ مَلَكٌ ۖ وَلَوْ أَنزَلْنَا مَلَكًا لَّقُضِىَ ٱلْأَمْرُ ثُمَّ لَا يُنظَرُونَ
Na walisema, "Mbona hakuteremshiwa Malaika?" Na kama tungelimteremsha Malaika, basi bila ya shaka ingeshahukumiwa amri, kisha wasingelipewa muhula.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wao husema: Mbona hakuteremshiwa Malaika? Na kama tungeli teremsha Malaika, basi bila ya shaka ingesha hukumiwa amri, tena hapo wasingeli pewa muhula. [8]
[8] Tena wanasema: Tunataka Mwenyezi Mungu amteremshia Malaika huyu anaye dai Utume amsadikishe! Na lau kuwa Sisi tungeli waitikia hilo ombi lao, tukampeleka Malaika kama walivyo toa shauri, kisha wakafanya inda yao wasimuamini, basi amri ya kuwaangamiza ingesha pitishwa, tena hao wasinge pewa muhula hata chembe.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na walisema washirikina hawa, «Si Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Amteremshie Muhammad Malaika kutoka mbinguni ili amsadiki kwa yale aliyokuja nayo ya utume.» Na lau tungemteremsha Malaika kutoka mbinguni kwa kujibu ombi lao, uamuzi wa kuwaangamiza ungalipitishwa, na wasingepewa muhula wa kutubia, kwani imetangulia kwenye ujuzi wa Allah Mtukufu kuwa wao hawataamini.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net