Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 9

Al-An'aam 6:9

الأنعام

وَلَوْ جَعَلْنَـٰهُ مَلَكًا لَّجَعَلْنَـٰهُ رَجُلًا وَلَلَبَسْنَا عَلَيْهِم مَّا يَلْبِسُونَ

Maana

Na kama tungelimfanya Malaika, bila ya shaka tungelimfanya kuwa mwanamume, na tungeliwatilia matatizo yale wanayoyatatiza wao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kama tungeli mfanya Malaika bila ya shaka tungeli mfanya kama binaadamu, na tungeli watilia matatizo yale wanayo yatatiza wao. [9]

[9] Na lau kuwa tunge jaalia huyo wa kumuunga mkono Mtume ni Malaika kama watakavyo hao, basi tungeli mfanya katika sura ya mwanaadamu, ili wapate kumwona na kufahamiana naye. Kwani wao hawawezi kumwona Malaika katika sura yake ya asili. Tena mambo yangeli watatiza na kuwadanganyikia kwa kupelekwa kwa sura ya mwanaadamu, na tungeli watia katika makosa yale yale yalio wazonga. Kauli hii inaashiria maana ambayo wenye ilimu za kisasa wanaitaja. Wenye ilimu za mambo ya kiroho wanasema kuwa roho zina mwili khafifu, mwembamba na mwepesi, mfano wa ng'amba. Nazo hazidhihiri wala hazionekani. Na hayumkiniki kuonekana roho ila zikivaa huo mwili. Na Malaika hawana kiwiliwili. Katika viumbe vyote vya kiroho Malaika ndio khafifu kabisa kushinda vyote. Na hayumkini kuonekana ila kwa sura ya mwili. Na huu mwili ndio unakuwa kama mwanaadamu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kama tungalimfanya mtume aliyeteremshwa kwao ni Malaika, kwani hawakukinai na Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie) (tungalimfanya Malaika huyo kwenye sura za mwanadamu) ili waweze kumsikia na kusema naye. Kwani haimkiniki kwao kumuona Malaika katika sura zake za kimalaika. Na lau Malaika angewajia kwa sura za binadamu, jambo hilo lingaliwafanya wachanganyikiwe kama lilivyowafanya wachanganyikiwe jambo la Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie.)

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net