Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 10

Al-An'aam 6:10

الأنعام

وَلَقَدِ ٱسْتُهْزِئَ بِرُسُلٍ مِّن قَبْلِكَ فَحَاقَ بِٱلَّذِينَ سَخِرُوا۟ مِنْهُم مَّا كَانُوا۟ بِهِۦ يَسْتَهْزِءُونَ

Maana

Na hakika walifanyiwa mzaha Mitume waliokuwa kabla yako, lakini wale waliowafanyia mzaha yakawafika yale yale waliyokuwa wakiyafanyia mzaha.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hakika Mitume walio kabla yako walifanyiwa kejeli, lakini walio wafanyia kejeli wakaja kuzungukwa na yale yale waliyo kuwa wao wanayafanyia kejeli. [10]

[10] Ewe Nabii! Makafiri waliwafanyia maskhara mengi Mitume wa kabla yako. Adhabu waliyo waonya nayo Mitume wao iliwazunguka hao wafanyao maskhara. Na kwanza hayo ndio waliyo kuwa wakiyakejeli.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kwa kuwa kutaka kwao kuteremshwa Malaika kulikuwa ni kwa njia ya kumfanyia shere Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie,) Allah Mtukufu, (Aliyetukuka,) Aliwaelezea kwamba kuwafanyia shere Mitume, (amani iwashukie,) si jambo jipya; kwani jambo hilo lilitokea kwa makafiri waliopita kuwafanyia Mitume wao, wakazungukwa na adhabu ambayo walikuwa wakiifanyia shere na wakipinga kuja kwake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net