Al-An'aam 6:11
الأنعامقُلْ سِيرُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ ثُمَّ ٱنظُرُوا۟ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ ٱلْمُكَذِّبِينَ
Sema: Tembeeni katika ardhi, kisha mtazame vipi ulikuwa mwisho wa wanaokadhibisha.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Tembeeni ulimwenguni, kisha mtazame ulikuwaje mwisho wa wanao kanusha. [11]
[11] Ewe Nabii! Waambie hawa makafiri: Nendeni pande zote duniani, mzingatie vipi maangamio yalivyo kuwa mwisho wa wanao wakanusha Mitume wao. Uzingatieni vyema mwisho huu na khatima hiyo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema kuwaambia: ewe Mtume, «nendeni katika ardhi kisha muangalie: namna gani Allah Mtukufu aliwaletea maangamivu na hizaya mwishoni! Basi tahadharini yasiwafikie mfano wa maanguko yao, na ogopeni yasije yakawashukia nyinyi kama yale yaliyowashukia wao».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net