Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 12

Al-An'aam 6:12

الأنعام

قُل لِّمَن مَّا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۖ قُل لِّلَّهِ ۚ كَتَبَ عَلَىٰ نَفْسِهِ ٱلرَّحْمَةَ ۚ لَيَجْمَعَنَّكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ ٱلْقِيَـٰمَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۚ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ

Maana

Sema: Ni vya nani vilivyo katika mbingu na katika ardhi? Sema: Ni vya Mwenyezi Mungu. Yeye ameiandika rehema juu ya nafsi yake. Hakika atawakusanya hadi Siku ya Kiyama isiyokuwa na shaka. Wale waliojihasiri nafsi zao, wao hawaamini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Ni vya nani viliomo katika mbingu na katika ardhi? Sema: Ni vya Mwenyezi Mungu. Yeye amejilazimisha nafsi yake kurehemu. Hakika atakukusanyeni Siku ya Kiyama isiyo kuwa na shaka. Walio jikhasiri wenyewe hawaamini. [12]

[12] Ewe Nabii! Waambie hawa wapinzani: Nani Mmiliki mbingu na ardhi, na viliomo ndani yao? Wakiemewa, wape jawabu ambayo hakuna nyengineyo, nayo ni: Hakika Mwenye kuvimiliki vyote hivyo ni Mwenyezi Mungu peke yake, wala hana mshirika. Na Yeye amejiwajibishia Mwenyewe rehema kuwarehemu waja wake. Kwa hivyo hawafanyii haraka kuwaadhibu, na anakubali toba yao. Hakika, atakukusanyeni Siku ya Kiyama ambayo haina shaka. Walio zipoteza nafsi zao, na wakazipelekea kwenye adhabu katika Siku hii, ni wale ambao hawamsadiki Mwenyezi Mungu, wala Siku ya Hisabu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Ni ya nani mamlaka ya mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake?» Sema, «Ni ya Allah Mtukufu. Na kama mnavyolikubali hilo na kulijua, basi muabuduni Yeye Peke Yake. Allah Mtukufu Amechukua ahadi juu ya nafsi Yake kurehemu, Hatawaangamiza waja Wake kwa kuwatesa. Kwa hakika Atakukusanyeni Siku ya Kiyama ambayo haina shaka ili mhesabiwe na mlipwe. Wale waliomshirikisha Allah Mtukufu wamejiangamiza nafsi zao; wao hawampwekeshi Allah Mtukufu wala hawaiamini ahadi Yake ya Pepo na Moto na hawaukubali unabii wa Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie).

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net