Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 13

Al-An'aam 6:13

الأنعام

وَلَهُۥ مَا سَكَنَ فِى ٱلَّيْلِ وَٱلنَّهَارِ ۚ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ

Maana

Na ni vyake vilivyotulia katika usiku na mchana. Naye ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kujua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ni vyake vilio tulia usiku na mchana. Naye ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua. [13]

[13] Ni vya Mwenyezi Mungu vya kila zama, kama ilivyo kuwa vyake vya kila pahala. Naye ndiye Mwenye kusikia kila la kusikiwa, na Mwenye kujua kila la kujuulikana.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ni wa Allah Mtukufu umiliki wa kila kitu, kilicho mbinguni na ardhini, kilichotulia na kinachotembea, kilichofichika na kilicho wazi. Vyote ni watumwa Wake na viumbe Vyake na viko chini ya utendeshaji nguvu Wake, uendeshaji Wake na upangaji Wake. Yeye Ndiye Msikizi wa maneno ya waja Wake, Ndiye Mjuzi wa siri zao na matendo yao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net