Al-An'aam 6:14
الأنعامقُلْ أَغَيْرَ ٱللَّهِ أَتَّخِذُ وَلِيًّا فَاطِرِ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَهُوَ يُطْعِمُ وَلَا يُطْعَمُ ۗ قُلْ إِنِّىٓ أُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ أَوَّلَ مَنْ أَسْلَمَ ۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلْمُشْرِكِينَ
Sema: Je, nimfanye rafiki mwandani asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Muumba mwanzilishi wa mbingu na ardhi, naye ndiye anayelisha wala halishwi? Sema: Hakika Mimi nimeamrishwa kwamba niwe wa kwanza wa wenye kusilimu. Na wala kabisa usiwe miongoni wa washirikina.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Je, nimchukue rafiki mlinzi asiye kuwa Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Muumba mbingu na ardhi, naye ndiye anaye lisha wala halishwi? Sema: Mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza wa wenye kusilimu. Na wala kabisa usiwe miongoni wa washirikina. [14]
[14] Sema ewe Nabii! Mimi simfanyi yeyote kuwa ni mungu na msaidizi isipo kuwa Mwenyezi Mungu, Allah, tu. Yeye peke yake ndiye aliye ziumba tangu mwanzo mbingu na ardhi kwa nidhamu isiyo kuwa na kiigizo kilicho tangulia. Naye ndiye Mwenye kuwaruzuku chakula waja wake, wala Yeye hahitaji kwao chakula. Sema: Hakika Mwenyezi Mungu ameniamrisha niwe wa mwanzo wa kusilimu, na amenikataza kumshirikisha Yeye na yeyote mwenginewe katika kumuabudu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa wanaomshirikisha Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na asiyekuwa Yeye, «Je, nimchukue asiyekuwa Allah Mtukufu kuwa ni msaidizi na ni mwokozi, na hali Yeye ni Muumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, na Yeye Ndiye Mwenye kuwaruzuku viumbe Wake na hakuna mwenye kumruzuku Yeye?» Sema,ewe Mtume, «Mimi nimeamrishwa niwe ni wa mwanzo aliyemnyenyekea Yeye na kumfuata katika umma huu. Na nimekatazwa kuwa ni miongoni mwa wanaomshirikisha Yeye na asiyekuwa Yeye».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net