Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 15

Al-An'aam 6:15

الأنعام

قُلْ إِنِّىٓ أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّى عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ

Maana

Sema: Hakika Mimi ninahofu nikimuasi Mola wangu Mlezi, adhabu ya Siku kubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Mimi naogopa adhabu ya Siku kubwa hiyo ikiwa nitamuasi Mola wangu Mlezi. [15]

[15] Sema: Mimi naogopa, nikenda kinyume na amri ya Mola Mlezi wangu na nikamuasi nisije nikapata adhabu ya hiyo Siku ya shida.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa wenye kumshirikisha Allah Mtukufu na asiyekuwa Yeye, Mimi naogopa nikimuasi Mola wangu, nikaenda kinyume na maamrisho Yake, na nikamshirikisha Yeye na asiyekuwa Yeye, kuteremkiwa na adhabu kubwa Siku ya Kiyama.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net