Al-An'aam 6:7
الأنعاموَلَوْ نَزَّلْنَا عَلَيْكَ كِتَـٰبًا فِى قِرْطَاسٍ فَلَمَسُوهُ بِأَيْدِيهِمْ لَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ إِنْ هَـٰذَآ إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ
Na lau tungelikuteremshia kitabu cha karatasi, wakakigusa kwa mikono yao, wangelisema wale waliokufuru: Haya si chochote isipokuwa ni uchawi ulio wazi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na lau tungeli kuteremshia kitabu cha karatasi, wakakigusa kwa mikono yao, wangeli sema walio kufuru: Haya si chochote ila ni uchawi dhaahiri. [7]
[7] Ewe Nabii! Hata tungeli kuteremshia dalili ya ujumbe wako iliyo andikwa katika karatasi, na wao wakaiona kwa macho yao, na wakahakikisha kwa kuiwekea mikono yao juu yake, basi pia wangeli sema kwa chuki tu: Hichi tunacho kigusa si chochote ila ni uchawi tu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na lau tungekuteremshia kitabu kutoka mbinguni, katika kurasa, wakazigusa washirikina hawa kwa mikono yao, wangesema, «Uliokuja nao ni uchawi ulio wazi uliobainika».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net