Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 65

Al-An'aam 6:65

الأنعام

قُلْ هُوَ ٱلْقَادِرُ عَلَىٰٓ أَن يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عَذَابًا مِّن فَوْقِكُمْ أَوْ مِن تَحْتِ أَرْجُلِكُمْ أَوْ يَلْبِسَكُمْ شِيَعًا وَيُذِيقَ بَعْضَكُم بَأْسَ بَعْضٍ ۗ ٱنظُرْ كَيْفَ نُصَرِّفُ ٱلْـَٔايَـٰتِ لَعَلَّهُمْ يَفْقَهُونَ

Maana

Sema: Yeye ndiye Muweza wa kuwatumia adhabu kutoka juu yenu au kutoka chini ya miguu yenu, au awavishe fujo la mfarakano, na awaonjeshe baadhi yenu jeuri ya wenzi wenu. Tazama vipi tunavyozieleza Aya ili wafahamu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Yeye ndiye Muweza wa kukuleteeni adhabu kutoka juu yenu au kutoka chini ya miguu yenu, au kukuleteeni fujo la mfarakano, na kuwaonjesha baadhi yenu jeuri ya wenzao. Tazama vipi tunavyo zieleza Aya ili wapate kufahamu. [65]

[65] Sema: Hakika ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye awezaye kukuleteeni adhabu kutoka juu yenu au chini yenu, au kukufanyeni nyinyi kwa nyinyi mkawa maadui, mkawa mataifa yenye kuwa mbali mbali matamanio yao, yenye kuchukiana, mkitesana nyinyi kwa nyinyi kwa mateso machungu na makali! Angalia vipi hoja zinavyo onyesha uwezo wetu na kustahiki kwetu peke yetu kuabudiwa, ili wapate kuzingatia na kuifahamu Haki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, «Allah Mtukufu, Aliyeshinda na kutukuka, Ndiye Muweza, Peke Yake, kuwatumia adhabu kutoka juu yenu, kama kupigwa mawe au mvua ya mafuriko na mfano wake, au kutoka chini ya miguu yenu, kama mitetemeko ya ardhi na kuzama ndani ardhi, au Awavurugie mambo yenu muwe makundi yanayozozana, mnauana nyinyi kwa nyinyi,» Angalia, ewe Mtume, vipi tunazifanya aina mbalimbali hoja zetu zilizo wazi kwa hawa washirikina ili waelewe na wazingatie!

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net