Al-An'aam 6:66
الأنعاموَكَذَّبَ بِهِۦ قَوْمُكَ وَهُوَ ٱلْحَقُّ ۚ قُل لَّسْتُ عَلَيْكُم بِوَكِيلٍ
Na kaumu yako waliikadhibisha, nayo ndiyo Haki. Sema: Mimi si wakili juu yenu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na watu wako wameikanusha, nayo ni Haki. Sema: Mimi sikuwakilishwa juu yenu. [66]
[66] Na kaumu yako wameikanusha Qur'ani, nayo ni Haki ambayo haina cha kukanushwa ndani yake. Ewe Nabii! Waambie: Mimi sikuwekwa kuwa ni muwakilishi wa kukulindeni, na kupima vitendo vyenu na kukulipeni kwavyo. Bali mambo yenu katika hayo yako kwa Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na waliikanusha hii Qur’ani makafiri kati ya watu wako, ewe Mtume; nayo ni kitabu chenye ukweli katika kila kilichokuja nacho, Waambie, «Mimi si mlinzi wala mtunzi juu yenu. Mimi ni mjumbe wa Allah Mtukufu, nawafikishia nyinyi yale niliotumwa nayo kwenu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net