Al-An'aam 6:64
الأنعامقُلِ ٱللَّهُ يُنَجِّيكُم مِّنْهَا وَمِن كُلِّ كَرْبٍ ثُمَّ أَنتُمْ تُشْرِكُونَ
Sema: Mwenyezi Mungu hukuokoeni kutoka katika hayo, na kutoka katika kila mashaka, na kisha nyinyi mnamshirikisha!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Mwenyezi Mungu hukuokoeni kutoka hayo, na kutoka kila mashaka, na kisha nyinyi mnamshirikisha! [64]
[64] Sema: Ni Allah, Mwenyezi Mungu wa pekee, ndiye aliye kuokoeni na vitisho hivi, na kila shida nyengineyo. Na kisha nyinyi pamoja na hayo mnamshirikisha na wengine katika ibada, ambao hawawezi kuondoa shari wala kuleta kheri!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Waambie, ewe Mtume, «Allah Mtukufu, Peke Yake, Ndiye Mwenye kuwaokoa na vitisho hivyo na kila tatizo, kisha nyinyi baada ya hapo mnawashirikisha wengine pamoja Naye katika ibada».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net