Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 63

Al-An'aam 6:63

الأنعام

قُلْ مَن يُنَجِّيكُم مِّن ظُلُمَـٰتِ ٱلْبَرِّ وَٱلْبَحْرِ تَدْعُونَهُۥ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً لَّئِنْ أَنجَىٰنَا مِنْ هَـٰذِهِۦ لَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلشَّـٰكِرِينَ

Maana

Sema: Ni nani anayewaokoa kutoka katika giza la nchi kavu na baharini? Mnamwomba kwa unyenyekevu na kwa siri, mkisema: Kama akituokoa na haya, bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Ni nani anaye kuokoeni katika giza la nchi kavu na baharini? Mnamwomba kwa unyenyekevu na kwa siri, mkisema: Kama akituokoa na haya bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa wanao shukuru. [63]

[63] Ewe Nabii! Waambie washirikina: Nani anaye kuvueni na vitisho vya bara na baharini vinapo kutokeeni, mkamuaungukia na mkamwomba kwa unyenyekevu wa dhaahiri na wa ndani, mkisema: Tunaapa! Kama ukituvua na vitisho hivi tutakuwa katika wanao kiri fadhila yako, na wanao dumu kukushukuru?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Waambie, ewe Mtume, hawa washirikina, «Ni nani mwenye kuwaokoa na vitisho vya giza vya bara na bahari? Kwani si Allah Mtukufu mnayemuomba kwenye matatizo mkionesha unyonge wenu kwa dhahiri na kwa siri? Huwa mkisema, ‘Hakika Mola wetu Akituokoa na vitisho hivi, tutakuwa ni wenye kushukuru kwa kumuabudu, Aliyeshinda na kutukuka, Peke Yake, Asiye na mshirika».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net