Al-An'aam 6:62
الأنعامثُمَّ رُدُّوٓا۟ إِلَى ٱللَّهِ مَوْلَىٰهُمُ ٱلْحَقِّ ۚ أَلَا لَهُ ٱلْحُكْمُ وَهُوَ أَسْرَعُ ٱلْحَـٰسِبِينَ
Kisha watarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, Mola wao wa Haki. Hakika, hukumu ni yake. Naye ni Mwepesi zaidi kuliko wote wanaohisabu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kisha watarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, Mola wao wa Haki. Hakika, hukumu ni yake. Naye ni Mwepesi kuliko wote wanao hisabu. [62]
[62] Tena hawa maiti watafufuliwa Siku ya Kiyama, na watasimamishwa mbele ya Mola Mlezi wao ambaye ndiye anayatawala mambo yao peke yake. Jueni kuwa Yeye tu ndiye wa kuamua baina ya viumbe na kuwahisabu katika Siku hiyo, naye ni Mwepesi wa kuhisabu na kulipa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kisha hawa waliokufa watarudishwa kwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Mola wao wa kweli. Jua utanabahi kwamba hukumu na uamuzi baina ya waja Wake, Siku ya Kiyama, ni Vyake Yeye tu. Na Yeye Ndiye mwepesi wa wenye kuhesabu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net