Al-An'aam 6:61
الأنعاموَهُوَ ٱلْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِۦ ۖ وَيُرْسِلُ عَلَيْكُمْ حَفَظَةً حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَ أَحَدَكُمُ ٱلْمَوْتُ تَوَفَّتْهُ رُسُلُنَا وَهُمْ لَا يُفَرِّطُونَ
Naye ndiye Mwenye nguvu za kushinda, aliye juu ya waja wake. Na huwapelekea (nyinyi) waangalizi, mpaka mmoja wenu yakimjia mauti wajumbe wetu humfisha, nao hawapuuzi chochote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Naye ndiye Mwenye nguvu za kushinda, aliye juu ya waja wake. Na hukupelekeeni waangalizi, mpaka mmoja wenu yakimjia mauti wajumbe wetu humfisha, nao hawafanyi taksiri. [61]
[61] Naye ndiye Mwenye kushinda kwa uwezo wake, aliye tukuka kwa ufalme wake juu ya waja wake, na anaye kupelekeeni Malaika wa kudhibiti kila vitendo vyenu, mpaka ufike mwisho wa kila mmoja wenu, ishikwe roho yake na Malaika wetu tunao wapeleka kwa kazi hiyo. Na wao hao Malaika hawafanyi taksiri katika kazi walio wakilishwa kuitenda.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Ndiye Al-Qãhir (Mtendesha nguvu), Aliye juu ya waja Wake, ujuu wa kila namna usio na mipaka unaonasibiana na utukufu Wake, kutakasika na kila sifa mbaya ni Kwake na kutukuka ni Kwake. Kila kitu kinaunyenyekea utukufu Wake na ukubwa Wake. Yeye Anawatuma kwa waja Wake Malaika kuyadhibiti matendo yao na kuyahesabu. Mpaka kifo kinapomshukia mmoja wao, Malaika wa mauti na wasaidizi wake wanaichukua roho yake, na wao hawaachi kutekeleza walichoamrishwa kukifanya.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net