Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 60

Al-An'aam 6:60

الأنعام

وَهُوَ ٱلَّذِى يَتَوَفَّىٰكُم بِٱلَّيْلِ وَيَعْلَمُ مَا جَرَحْتُم بِٱلنَّهَارِ ثُمَّ يَبْعَثُكُمْ فِيهِ لِيُقْضَىٰٓ أَجَلٌ مُّسَمًّى ۖ ثُمَّ إِلَيْهِ مَرْجِعُكُمْ ثُمَّ يُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ

Maana

Naye ndiye anayewafisha usiku, na anakijua mlichokifanya mchana. Kisha Yeye huwafufua humo mchana ili muda uliowekwa utimizwe. Kisha kwake Yeye ndiyo marejeo yenu, kisha atawaambia yale mliyokuwa mkiyafanya.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Naye ndiye anaye kufisheni usiku, na anakijua mlicho fanya mchana. Kisha Yeye hukufufueni humo mchana ili muda ulio wekwa utimizwe. Kisha kwake Yeye ndiyo marejeo yenu, na tena akwambieni mliyo kuwa mkiyafanya. [60]

[60] Na Yeye ndiye anakulazeni usiku, na anakuamsheni mchana. Na anajua mnayo yachuma, mpaka utimie muda wa kumfikia kila mmoja wenu ajali yake duniani ya kufa. Kisha Siku ya Kiyama mtarejeshwa nyote nyinyi kwa Mwenyezi Mungu peke yake. Tena atakwambieni a'mali zenu mlizo tenda duniani, njema au mbaya, na akulipeni kwazo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Anayezichukua roho zenu usiku kwa namna inayofanana na vile roho hizo zinachukuliwa kipindi cha kifo, na Anayajua matendo mnayoyafanya mchana, kisha Anazirudisha roho zenu kwenye miili yenu kwa kuamka kutoka usingizini kipindi cha mchana kwa namna inayofanana na kuhuisha baada kufa, ili umalizike muda maalumu uliowekwa wa maisha yenu ulimwenguni. Kisha marejeo yenu ni kwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, baada ya kufufuliwa kwenu kutoka kwenye makaburi yenu mkiwa hai. Kisha Atawaelezea yale mliokuwa mkiyafanya kipindi cha maisha yenu ya ulimwengu. Kisha Atawalipa kwa hayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net