Al-An'aam 6:59
الأنعاموَعِندَهُۥ مَفَاتِحُ ٱلْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَآ إِلَّا هُوَ ۚ وَيَعْلَمُ مَا فِى ٱلْبَرِّ وَٱلْبَحْرِ ۚ وَمَا تَسْقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلَّا يَعْلَمُهَا وَلَا حَبَّةٍ فِى ظُلُمَـٰتِ ٱلْأَرْضِ وَلَا رَطْبٍ وَلَا يَابِسٍ إِلَّا فِى كِتَـٰبٍ مُّبِينٍ
Na ziko kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Yeye anajua kilicho katika nchi kavu na baharini. Na halidondoki jani ila analijua. Wala punje katika giza la ardhi, wala kinyevu, wala kikavu ila kimo katika Kitabu kinachobainisha.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ziko kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Yeye anajua kilioko nchi kavu na baharini. Na halidondoki jani ila analijua. Wala punje katika giza la ardhi, wala kinyevu, wala kikavu ila kimo katika Kitabu kinacho bainisha. [59]
[59] Ni Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye ujuzi wa milango yote ya vilio ghaibu, visio juulikana na wengine. Hapana Mwenye kukusanya ujuzi wa hivyo ila Yeye, na anao wataka kuwapa baadhi yake. Naye ujuzi wake umekusanya vitu vyote vilioko nchi kavu na vilioko baharini. Wala halidondoki jani, jani lolote lile, ila Yeye analijua, wala haianguki mbegu chini ya ardhi, wala chochote kilicho kinyevu au kikavu, ila Yeye Subhanahu anakijua kwa utimilifu. Kauli hii inafahamisha kuwa kujua mambo ya ghaibu kuko kwa Mwenyezi Mungu, na funguo za hayo ziko kwake tu. Na mambo ya ghaibu ni mafungu mawili: Ghaibu Mut'laq ambayo hayumkini kutambulikana na akili, kama mambo yatakayo mfikia mtu katika mustakbali. Na Ghaib Nisbiy hizi ni siri za ulimwengu na viliomo ndani yake, na kuweza kuvitumia kwa maslaha ya watu. Ujuzi wa hayo huweza kughibu kwa vizazi kadhaa, kisha ukadhihiri.. Na funguo ya hizi pia ziko kwa Mwenyezi Mungu, humwezesha amtakaye katika waja wake wale wanao zama kuusoma ulimwengu. Na katika hayo ni haya ya uvumbuzi ambao tunauona anao ufikilia mwanaadamu kwa kuwezeshwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka na kuwa juu, kuna mafãtih( al-ghayb, yaani: hazina za mambo ya ghaibu yaliyofichika, hakuna azijuwazo ila Yeye. Miongoni mwazo ni ujuzi wa Kiyama, kuteremka mvua, viliyomo ndani ya zao, matendo ya siku zinazokuja na mahala mtu atakapokufa. Na Anajua kila kilichoko barani na baharini. Na hakuna jani, linaloanguka kutoka kwenye mmea wowote, isipokuwa Yuwalijua. Na kila chembe iliyofichika ardhini na kila kibichi na kikavu, kimethibitishwa kwenye kitabu kilicho wazi kisicho na utatizi nacho ni Al-Lawh Al-Maḥfûẓ (Ubao Uliohifadhiwa)
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net