Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 58

Al-An'aam 6:58

الأنعام

قُل لَّوْ أَنَّ عِندِى مَا تَسْتَعْجِلُونَ بِهِۦ لَقُضِىَ ٱلْأَمْرُ بَيْنِى وَبَيْنَكُمْ ۗ وَٱللَّهُ أَعْلَمُ بِٱلظَّـٰلِمِينَ

Maana

Sema: Lau kuwa ninacho hicho mnachotaka kije haraka, ingelikwishakatwa shauri baina yangu na nyinyi. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayewajua zaidi madhalimu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Lau kuwa ninacho hicho mnacho kihimiza, ingeli kwisha katwa shauri baina yangu na nyinyi. Na Mwenyezi Mungu anawashinda wote kuwajua madhaalimu. [58]

[58] Sema: Lau ingeli kuwa kumo katika makadara yangu kukuteremshieni hiyo adhabu mnayo ihimiza ije, ningeli kuteremshieni kwa kukasirika kwa ajili ya Mola Mlezi wangu. Na hapo mambo yangeli kwisha baina yangu na nyinyi. Walakini amri ni ya Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mwenye kujua kuliko wote wanayo stahiki makafiri katika adhabu ya haraka, au ya kuakhirika.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, Lau mimi nina mamlaka ya kuwateremshia adhabu ambayo mnaitaka kwa haraka, ningaliiteremsha kwenu, na uamuzi, baina yangu mimi na nyinyi, ungalitoka. Lakini hilo liko kwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka. Na Yeye Anawajua zaidi madhalimu ambao wamepita mipaka yao wakawashirikisha wengine pamoja na Yeye.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net