Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 57

Al-An'aam 6:57

الأنعام

قُلْ إِنِّى عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّى وَكَذَّبْتُم بِهِۦ ۚ مَا عِندِى مَا تَسْتَعْجِلُونَ بِهِۦٓ ۚ إِنِ ٱلْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ ۖ يَقُصُّ ٱلْحَقَّ ۖ وَهُوَ خَيْرُ ٱلْفَـٰصِلِينَ

Maana

Sema: Mimi nipo kwenye sheria iliyo wazi itokayo kwa Mola wangu Mlezi, nanyi mnaikanusha. Mimi sina hicho (adhabu) mnachotaka kije haraka. Hakuna hukumu ila ya Mwenyezi Mungu. Yeye anasimulia yaliyo kweli; naye ni Mbora wa kuhukumu kuliko wote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Mimi nipo kwenye sharia iliyo wazi itokayo kwa Mola wangu Mlezi, nanyi mnaikanusha. Mimi sinacho hicho mnacho kihimiza. Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu. Yeye anasimulia yaliyo kweli; naye ni Mbora wa kuhukumu kuliko wote. [57]

[57] Waambie: Mimi nipo juu ya Sharia iliyo wazi, iliyo teremshwa kutoka kwa Mola wangu Mlezi. Na nyinyi mmeikanusha Qur'ani iliyo ileta Sharia hii. Na mimi sina uwezo kuileta hiyo adhabu mnayo ihimiza ije. Bali hayo yamo katika uwezo wa Mwenyezi Mungu, na yamelazimika na kupenda kwake na hikima yake. Na hakuna amri wala madaraka ila ya Mwenyezi Mungu tu. Akipenda Yeye atakuleteeni adhabu kwa haraka, na akipenda ataichelewesha. Yeye Subhanahu, Aliye takasika, anafuata katika hayo hikima yake, naye ni mbora wa kuhukumu baina yangu na nyinyi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Mimi niko kwenye hoja iliyo wazi ya sheria ya Allah Mtukufu Aliyoniletea kwa njia ya wahyi. Nayo ni kumpwekesha Allah Mtukufu Peke Yake kwa ibada. Na hili mlilikanusha. Na haliko kwenye uwezo wangu jambo la kuwateremshia adhabu mnayoitaka kwa haraka. Na uamuzi wa kuchelewesha hilo uko tu kwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka. Yeye Anahadithia ukweli na Yeye Ndiye bora wa kupambanua baina ya haki na batili kwa uamuzi Wake na hukumu Yake».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net