Al-An'aam 6:51
الأنعاموَأَنذِرْ بِهِ ٱلَّذِينَ يَخَافُونَ أَن يُحْشَرُوٓا۟ إِلَىٰ رَبِّهِمْ ۙ لَيْسَ لَهُم مِّن دُونِهِۦ وَلِىٌّ وَلَا شَفِيعٌ لَّعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ
Na waonye kwayo wale wanaohofu kuwa watakusanywa kwa Mola wao Mlezi, hali ya kuwa hawana kando naye mlinzi wala mwombezi, ili wamche Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na waonye kwayo wanao ogopa kuwa watakusanywa kwa Mola wao Mlezi, hali kuwa hawana mlinzi wala mwombezi isipo kuwa Yeye, ili wapate kuchamngu. [51]
[51] Na wahadharishe kwa yaliyomo katika hii Qur'ani wale wanayo khofu vitisho vya Siku watapo wachunga Malaika kwa ajili ya hisabu na malipo, Siku ambayo itayo kuwa haina wa kunusuru wala kuombea ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, wahadharishe wajitenge mbali na vinavyo mkasirisha Mwenyezi Mungu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na waonyo, ewe Mtume, kwa hii Qur’ani wale ambao wanajua kuwa wao watafufuliwa wapelekwe kwa Mola wao. Wao wanaiyamini ahadi ya Allah Mtukufu ya kuwalipa mema wenye kufanya wema na kuwalipa maovu wenye kufanya uovu. Wao hawana, isipokuwa Allah Mtukufu, mtegemewa mwenye kuwanusuru wala muombezi mwenye kuwaombea mbele Yake Aliyetukuka Akawaokoa na adhabu Yake. Kwani huenda wao wakamcha Allah Mtukufu, Aliyetukuka, kwa kuyafanya maamrisho na kuyaepuka makatazo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net