Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 52

Al-An'aam 6:52

الأنعام

وَلَا تَطْرُدِ ٱلَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِٱلْغَدَوٰةِ وَٱلْعَشِىِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُۥ ۖ مَا عَلَيْكَ مِنْ حِسَابِهِم مِّن شَىْءٍ وَمَا مِنْ حِسَابِكَ عَلَيْهِم مِّن شَىْءٍ فَتَطْرُدَهُمْ فَتَكُونَ مِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Maana

Wala usiwafukuze wale wanaomwomba Mola wao Mlezi asubuhi na jioni kwa kutaka radhi yake. Si juu yako hisabu yao hata kidogo, wala hisabu yako si juu yao hata kidogo, hata uwafukuze na uwe miongoni mwa wenye kudhulumu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala usiwafukuze wanao mwomba Mola Mlezi wao asubuhi na jioni kwa kutaka radhi yake. Si juu yako hisabu yao hata kidogo, wala hisabu yako si juu yao hata kidogo, hata uwafukuze na uwe miongoni mwa wenye kudhulumu. [52]

[52] Na ewe Nabii! Usiitikie wito wa makafiri walio panda vichwa, ukawatenga Waumini wanyonge, wanao muabudu Mwenyezi Mungu daima, wala hawatafuti ila radhi zake. Wala usivishughulikie vitimbi vya washirikina juu ya hawa Waumini. Kwani wewe mbele ya Mwenyezi Mungu huna jukumu juu ya vitendo vyao, kama wao wasivyo kuwa na jukumu juu ya chochote katika vitendo vyako. Na ukiwakubalia hawa makafiri wenye kani, na ukawatenga Waumini, utakuwa miongoni mwa walio dhulumu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na usiwatenge, ewe Nabii, kukaa na wewe Waislamu wanyonge wanaomuabudu Mola wao mwanzo wa mchana na mwisho wake, hali wakitaka, kwa matendo yao mema, radhi za Allah Mtukufu. Kitu chochote kuhusu hesabu ya maskini hawa hakiko juu yako; hesabu yao iko juu ya Allah Mtukufu. Na si juu yao chochote kuhusu hesabu yako. Basi ukiwatenga, utakuwa ni miongoni mwa wenye kuivuka mipaka ya Allah Mtukufu, wenye kuweka vitu mahali pasipokuwa pake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net