Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 53

Al-An'aam 6:53

الأنعام

وَكَذَٰلِكَ فَتَنَّا بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لِّيَقُولُوٓا۟ أَهَـٰٓؤُلَآءِ مَنَّ ٱللَّهُ عَلَيْهِم مِّنۢ بَيْنِنَآ ۗ أَلَيْسَ ٱللَّهُ بِأَعْلَمَ بِٱلشَّـٰكِرِينَ

Maana

Na hivi ndivyo tunavyowajaribu wao kwa wao, ili waseme: Ni hao ndio Mwenyezi Mungu amewafadhilisha miongoni mwetu? Kwani Mwenyezi Mungu hawajui vyema wanaoshukuru?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hivi ndivyo tunavyo wajaribu wao kwa wao, ili waseme: Ni hao ndio Mwenyezi Mungu amewafadhilisha miongoni mwetu? Kwani Mwenyezi Mungu hawajui wanao shukuru? [53]

[53] Na kwa majaribio kama haya ambayo ndio ada yetu kuyatenda, tukawafanyia mtihani walio takabari kwa kuwatanguliza wanyonge wawe mbele kusilimu; wapate kusema wenye kiburi, wanao pinga, wakifanya kejeli: Hivyo ni hawa mafakiri ndio alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwetu sote kwa kuwapa hiyo kheri aliyo waahidi Muhammad? Hakika hawa mafakiri wanaijua neema ya Mwenyezi Mungu juu yao kwa kuwapa tawfiki ya kuifikia Imani, na kwa hivyo wanamshukuru. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua zaidi nani anashukuru fadhila yake na neema yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hivyo basi Allah Mtukufu Amewapa mtihani waja Wake kwa kutafautiana mafungu yao ya riziki na umbo, Akawafanya baadhi yao matajiri na wengine maskini, baadhi yao wenye nguvu na wengine madhaifu Na Akawafanya baadhi yao ni wahitaji wa wengine ili kuwajaribu kwa hilo, wapate makafiri matajiri kusema, «Ni madhaifu hawa, miongoni mwetu, Allah Mtukufu Amewapa neema ya Uislamu?» Kwani Allah Mtukufu, Aliyetukuka, si Mjuzi zaidi wa wanaoshukuru neema Yake Akawaafikia kwenye uongofu wa dini Yake?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net