Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 54

Al-An'aam 6:54

الأنعام

وَإِذَا جَآءَكَ ٱلَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِـَٔايَـٰتِنَا فَقُلْ سَلَـٰمٌ عَلَيْكُمْ ۖ كَتَبَ رَبُّكُمْ عَلَىٰ نَفْسِهِ ٱلرَّحْمَةَ ۖ أَنَّهُۥ مَنْ عَمِلَ مِنكُمْ سُوٓءًۢا بِجَهَـٰلَةٍ ثُمَّ تَابَ مِنۢ بَعْدِهِۦ وَأَصْلَحَ فَأَنَّهُۥ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Maana

Na wanapokujia wanaoziamini Ishara zetu waambie: Assalamu alaikum! (Amani iwe juu yenu!) Mola wenu Mlezi amejilazimisha rehema, ya kwamba atakayefanya uovu miongoni mwenu kwa ujinga, kisha akatubu baada yake na akatengenea, basi hakika Yeye ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanapo kujia wanao ziamini Ishara zetu waambie: Assalamu alaikum! Amani iwe juu yenu! Mola wenu Mlezi amejilazimisha rehema, ya kwamba atakaye fanya uovu miongoni mwenu kwa ujinga, kisha akatubu baada yake na akatengenea, basi hakika Yeye ni Mwenye maghfira na Mwenye kurehemu. [54]

[54] Na wakikujia wanao isadiki Qur'ani waambie kwa kuwahishimu: Assalamu Alaikum, Amani juu yenu. Nakubashirieni rehema kunjufu ya Mwenyezi Mungu, ambayo amejilazimisha Yeye Mwenyewe, kwa fadhila yake, na ambayo inahukumu kuwa yeyote katika nyinyi akitenda ubaya bila ya kuzingatia matokeo yake, kisha akarejea kwa Mwenyezi Mungu naye amejuta, ametubu, na akatengeneza a'mali zake, basi Mwenyezi Mungu atamghufiria, kwani Mwenyezi Mungu ni mwingi wa maghfira, na mkunjufu wa rehema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wakikujia, ewe Nabii, wale wanaoamini aya za Allah Mtukufu zenye kushuhudia ukweli wako juu ya Qur’ani na mengineyo, kutaka fat՚wa kuhusu toba ya madhambi yao yaliyotangulia, basi wakirimu kwa kuwarudishia salamu na uwape bishara ya rehema za Allah Mtukufu iliyo kunjufu. Kwani Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu, Ametoa ahadi Yake Mwenyewe kuwarehemu waja Wake kwa kuwafanyia wema kwamba mwenye kufanya dhambi kwa kutojua mwisho wake mbaya na kuwa linapelekea kukasirikiwa na Allah Mtukufu-Basi kila mwenye kumuasi Allah Mtukufu kwa kukosea au kwa kusudi huwa ni mjinga kwa mtizamo huu, ingawa ajua kuwa ni haramu- kisha baada yake akatubia na akaendelea kufanya matendo mema, basi Allah Mtukufu Atamsamehe dhambi zake, kwani Yeye ni Mwingi wa kusamehe kwa waja Wake wenye kutubia, ni Mwingi wa rehema kwao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net