Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 55

Al-An'aam 6:55

الأنعام

وَكَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ ٱلْـَٔايَـٰتِ وَلِتَسْتَبِينَ سَبِيلُ ٱلْمُجْرِمِينَ

Maana

Na ndivyo hivyo tunavyozieleza Ishara, na ili ibainike njia ya wahalifu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ndio hivi tunavyo zieleza Ishara ili ibainike njia ya wakosefu. [55]

[55] Na kwa mfano wa bayana hiyo iliyo wazi, tunaweka wazi dalili mbali mbali, ipate kudhihiri njia ya Haki wanayo ipitia Waumini, na ibainishe njia ya upotovu wanayo ipitia makafiri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mfano wa ufafanuzi huu tuliokufafanulia, tunakufafanulia, ewe Mtume, hoja zilizo wazi kwa kila mtu, ili ifunuke njia ya watu wa haki wanayoikanusha watu wa batili, na ifunuke njia ya watu wa batili wenye kuwaendea kinyume Mitume.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net