Al-An'aam 6:50
الأنعامقُل لَّآ أَقُولُ لَكُمْ عِندِى خَزَآئِنُ ٱللَّهِ وَلَآ أَعْلَمُ ٱلْغَيْبَ وَلَآ أَقُولُ لَكُمْ إِنِّى مَلَكٌ ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰٓ إِلَىَّ ۚ قُلْ هَلْ يَسْتَوِى ٱلْأَعْمَىٰ وَٱلْبَصِيرُ ۚ أَفَلَا تَتَفَكَّرُونَ
Sema: Mimi siwaambii kuwa ninazo hazina za Mwenyezi Mungu. Wala sijui mambo yaliyofichikana. Wala siwaambii kuwa mimi ni Malaika. Mimi sifuati isipokuwa yanayofunuliwa kwangu. Sema: Je, wanakuwa sawa, kipofu na mwenye kuona. Basi hamfikirii?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Mimi sikwambiini kuwa ninazo khazina za Mwenyezi Mungu. Wala sijui mambo yaliyo fichikana. Wala sikwambiini kuwa mimi ni Malaika. Mimi sifuati ila yanayo funuliwa kwangu. Sema: Je, wanakuwa sawa, kipofu na mwenye kuona. Basi hamfikiri? [50]
[50] Ewe Mtume! Waambie hawa makafiri: Mimi sikwambiini kuwa mimi nina madaraka aliyo nayo Mwenyezi Mungu hata nikuitikieni kwa mnayo yataka. Wala sidai kuwa mimi nina ilimu ya mambo ya ghaibu, ambayo Mwenyezi Mungu hakunijuvya. Wala sisemi kuwa mimi ni Malaika ninaweza kupanda mbinguni! Mimi si chochote ila ni mwanaadamu tu. Sifuati ila Mwenyezi Mungu anacho nifunulia. Sema ewe Nabii: Je, wanakuwa sawa, aliye potoka na aliye ongoka katika kuzijua kweli hizi? Hivyo, inakuelekeeni nyinyi mkautupa uwongofu ninao kuleteeni, msiuzingatie kwa akili zenu hata ikakubainikieni Haki?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina hawa, «Mimi sidai kuwa ninamiliki hazina za mbingu na ardhi nikawa ninazitumia nitakavyo; na sidai kuwa mimi najua al-ghayb (yasiyoonekana); na sidai kuwa mimi ni Malaika. Mimi ni Mtume kutoka kwa Allah Mtukufu, nafuata yale niliyoteremshiwa kwa njia ya wahyi na nawafikishia watu wahyi Wake.» Waambie, ewe Mtume, washirikina hawa. «Je, kafiri aliye kipofu wa kutoziona aya za Allah Mtukufu, Aliyetukuka, asiziamini yuko sawa na Muumini anayeziona aya za Allah Mtukufu na akaziamini? Kwani nyinyi hamzifikirii aya za Allah Mtukufu ili muione haki na muiamini?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net