Al-An'aam 6:49
الأنعاموَٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا يَمَسُّهُمُ ٱلْعَذَابُ بِمَا كَانُوا۟ يَفْسُقُونَ
Na wale waliozikadhibisha Ishara zetu itawagusa adhabu kwa vile walivyokuwa wakivuka mipaka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na walio kanusha Ishara zetu itawagusa adhabu kwa walivyo kuwa wakipotoka. [49]
[49] Na wale wanao zikanusha dalili zilio wazi za ukweli wa waliyo kuja nayo Mitume, watapata adhabu kwa kutoka kwao kwenye ut'iifu na Imani.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wale waliozikanusha aya zetu za Qur’ani na miujiza, hao itawapata adhabu Siku ya Kiyama kwa sababu ya ukafiri wao na kutoka kwao kwenye twaa ya Allah Mtukufu, Aliyetukuka.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net