Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 48

Al-An'aam 6:48

الأنعام

وَمَا نُرْسِلُ ٱلْمُرْسَلِينَ إِلَّا مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ ۖ فَمَنْ ءَامَنَ وَأَصْلَحَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ

Maana

Na hatuwatumi Mitume isipokuwa huwa ni wabashiri na waonyaji. Basi mwenye kuamini na akatengenea, haitakuwa hofu yoyote juu yao, wala hawatahuzunika.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hatuwatumi Mitume ila huwa ni wabashiri na waonyaji. Na wenye kuamini na wakatenda mema haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika. [48]

[48] Na Sisi hatuwatumi Manabii ila ni kwa ajili ya kuwabashiria wenye kuamini mambo ya kheri na thawabu, na kuwahadharisha na adhabu wale wanao kufuru. Basi wenye kuuamini wito wao, na wakatenda mema, hawatakuwa na khofu ya kuwapata shari, wala hawatahuzunika kwa kuikosa kheri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hatuwatumi wajumbe wetu isipokuwa wenye kuwapa bishara njema wenye kututii kuwa watakuwa na starehe ya daima, na kuwapa onyo wenye kuasi kuwa watakuwa na adhabu kali. Basi mwenye kuamini, akawasadiki mitume na akafanya mema, hao hawataogopa wakati wa kukutana na Mola wao wala hawatakuwa na masikitiko juu ya chochote walichokikosa miongoni mwa hadhi za kilimwengu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net