Al-An'aam
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
وَمَا نُرْسِلُ ٱلْمُرْسَلِينَ إِلَّا مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ ۖ فَمَنْ ءَامَنَ وَأَصْلَحَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ 48
{48} Yeye Mtukufu anataja kiini alichowatuma nacho Mitume, kuwa ni bishara na maonyo, na hilo linalazimu kufafanuliwa: mwenye bishara, na bishara yeyewe, na vitendo ambavyo mja akivifanya, anaipata bishara hii, na mwonyaji, na anayeonywa, na kinachoonywa dhidi yake, na matendo ambayo mwenye kuyafanya, atastahiki maonyo. Lakini watu waligawanyika kulingana na kuwalingania kwao na kutoitikia katika sehemu mbili: "Basi mwenye kuamini na akatengenea;" yaani, alimwamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Mwisho. Na akaifanya Imani yake kuwa nzuri, na vitendo vyake, na makusudio yake, "haitakuwa hofu yoyote juu yao," kuhusu yale yajayo; "wala hawatahuzunika" juu ya yale yaliyopita.