Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 42

Al-An'aam 6:42

الأنعام

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَآ إِلَىٰٓ أُمَمٍ مِّن قَبْلِكَ فَأَخَذْنَـٰهُم بِٱلْبَأْسَآءِ وَٱلضَّرَّآءِ لَعَلَّهُمْ يَتَضَرَّعُونَ

Maana

Na kwa yakini tuliwatuma Mitume kwa kaumu zilizokuwa kabla yako, kisha tukawatia katika dhiki na mashaka ili wanyenyekee.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kwa yakini tulipeleka Mitume kwa kaumu zilizo kuwa kabla yako, kisha tukazitia katika dhiki na mashaka ili zipate kunyenyekea. [42]

[42] Yasikudhiki, ewe Nabii, yanao kupata kwa watu wako. Kwani Sisi tuliwapeleka Mitume kabla yako kwa kaumu nyingi kabla ya umma wako huu, nao wakawaambia ni waongo. Nasi tukawapatiliza kwa adhabu zilizo wateremkia, na yaliyo wadhuru miili yao, ili walau wanyenyekee na warejee kwa Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika tuliwatuma, ewe Mtume, Wajumbe kuwaendea makundi ya watu kabla yako kuwalingania kwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, wakawakanusha na tukawapa mtihani katika mali yao, kwa ufukara mwingi na dhiki za maisha, na tukawapa mitihani katika miili yao, kwa magonjwa na kuumwa, ili wajidhalilishe kwa Mola wao na wanyenyekee Kwake Peke Yake kwa ibada.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net