Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 43

Al-An'aam 6:43

الأنعام

فَلَوْلَآ إِذْ جَآءَهُم بَأْسُنَا تَضَرَّعُوا۟ وَلَـٰكِن قَسَتْ قُلُوبُهُمْ وَزَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيْطَـٰنُ مَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ

Maana

Kwa nini hawakunyenyekea ilipowafika adhabu yetu? Lakini nyoyo zao zilikuwa ngumu, na Shetani akawapambia waliyokuwa wakiyafanya.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwa nini wasinyenyekee ilipo wafika adhabu yetu? Lakini nyoyo zao zilikuwa ngumu, na Shet'ani akawapambia waliyo kuwa wakiyafanya. [43]

[43] Na lililo takikana ni kuwa warejee kwa Mola wao Mlezi. Lakini hawakufanya hayo. Bali zikaendelea nyoyo zao katika ugumu wao, na Shetani akawapambia vile vitendo vyao vibaya, (wakaviona vizuri).

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi si ilipowajia, umma hawa wenye kukanusha, mitihani yetu ilitakiwa wajidhalilishe kwetu. Lakini wao nyoyo zao zilisusuwaa na Shetani aliwapambia yale ambayo waliokuwa wakiyafanya ya maasia na wakiyaleta ya ushirikina.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net