Al-An'aam 6:44
الأنعامفَلَمَّا نَسُوا۟ مَا ذُكِّرُوا۟ بِهِۦ فَتَحْنَا عَلَيْهِمْ أَبْوَٰبَ كُلِّ شَىْءٍ حَتَّىٰٓ إِذَا فَرِحُوا۟ بِمَآ أُوتُوٓا۟ أَخَذْنَـٰهُم بَغْتَةً فَإِذَا هُم مُّبْلِسُونَ
Basi waliposahau yale waliyokumbushwa, tuliwafungulia milango ya kila kitu. Mpaka walipofurahia yale waliyopewa, tukawashika kwa ghafla, na mara wakawa wenye kukata tamaa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi walipo sahau walio kumbushwa tuliwafungulia milango ya kila kitu. Mpaka walipo furahia yale waliyo pewa tuliwashika kwa ghafla, na mara wakawa wenye kukata tamaa. [44]
[44] Walipo acha kuwaidhika kwa ufakiri na maradhi tulio wapa kuwa ni mtihani, tukawajaribu baada yake kwa kuwapa riziki zenye wasaa. Tukawafungulia milango ya kila sababu za riziki, mpaka walipo furahia neema zetu, na wao wasimshukuru Mwenyezi Mungu kwa hayo, ikawajia adhabu ghafla. Wakawa wanadahadari, wamekata tamaa, hawaipati njia ya kuokoka.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi walipoacha kufuata amri za Allah Mtukufu, Aliyetukuka, kwa kuzipa mgongo, tuliwafungulia milango ya kila kitu miongoni mwa riziki, ndipo tukawabadilishia shida kwa kuwapa raha ya maisha, na tukawabadilishia magonjwa kwa kuwapa uzima wa miili, kwa kuwavuta kidogo kidogo. Hata watakapofanya kiburi na wakajiona kwa mema na neema tulizowapa, tutawashushia adhabu ya ghafla, wakitahamaki watajikuta wamekata tamaa wamekatika na kila zuri.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net