Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 45

Al-An'aam 6:45

الأنعام

فَقُطِعَ دَابِرُ ٱلْقَوْمِ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ ۚ وَٱلْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ

Maana

Ikakatwa mizizi ya kaumu waliodhulumu, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ikakatwa mizizi ya watu walio dhulumu - na wa kuhimidiwa ni Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote. [45]

[45] Ikateketezwa kabisa kaumu hii, yenye kudhulumu, asibakie hata mmoja. Alhamdulillahi, wa kuhimidiwa kwa sifa zote njema ni Mwenyezi Mungu, mwenye kuwalea viumbe kwa neema na nakama, na mwenye kuisafisha ardhi na ufisadi wa wenye kudhulumu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Watu hawa walimalizwa na kuangamizwa walipomkanusha Allah Mtukufu na kumkanusha Mtume Wake; hakuna yoyote aliyesalia kati yao. Shukrani na sifa njema ni za Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Muumba na Mwenye kumiliki kila kitu, kwa kuwapa ushindi mawalii Wake na kuwaangamiza maadui Zake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net