Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 46

Al-An'aam 6:46

الأنعام

قُلْ أَرَءَيْتُمْ إِنْ أَخَذَ ٱللَّهُ سَمْعَكُمْ وَأَبْصَـٰرَكُمْ وَخَتَمَ عَلَىٰ قُلُوبِكُم مَّنْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ ٱللَّهِ يَأْتِيكُم بِهِ ۗ ٱنظُرْ كَيْفَ نُصَرِّفُ ٱلْـَٔايَـٰتِ ثُمَّ هُمْ يَصْدِفُونَ

Maana

Sema: Mwaonaje Mwenyezi Mungu akinyakua kusikia kwenu, na kuona kwenu, na akaziziba nyoyo zenu, ni mungu gani asiyekuwa Mwenyezi Mungu atakayewaletea hayo tena? Angalia vipi tunavyozieleza Ishara, kisha wao wanapuuza.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Mwaonaje Mwenyezi Mungu akanyakua kusikia kwenu, na kuona kwenu, na akaziziba nyoyo zenu, ni mungu gani asiye kuwa Mwenyezi Mungu ataye kuleteeni hayo tena? Angalia vipi tunavyo zieleza Ishara, kisha wao wanapuuza. [46]

[46] Waambie, ewe Nabii: Hebu nambieni--Mwenyezi Mungu akinyakua kusikia kwenu, na akazifunika nyoyo zenu zisiweze kutambua kitu, akakufanyeni viziwi, vipofu hamfahamu kitu - mtamuabudu mungu gani isipo kuwa Mwenyezi Mungu atakae weza kukurejesheeni aliyo kunyang'anyeni Mwenyezi Mungu? Ewe Nabii! Tazama vipi tunavyo ziweka wazi hoja na kuzipanga mbali mbali. Kisha pamoja na haya wao wanakataa kuzizingatia na kunafiika kwazo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina hawa, «Nambieni ikiwa Allah Mtukufu atayaondoa masikizi yenu Akawafanya viziwi, Akayaondoa macho yenu Akawafanya vipofu na Akapiga mhuri juu ya nyoyo zenu mkawa hamfahamu neno, basi ni mola gani asiyekuwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka na kuwa juu, awezaye kuwarudishia nyinyi vitu hivyo?» Angalia, ewe Mtume, ni namna gani sisi tunawatolea hoja aina mbalimbali, kisha wao baada yake wanakataa kukumbuka na kuzingatia?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net