Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 41

Al-An'aam 6:41

الأنعام

بَلْ إِيَّاهُ تَدْعُونَ فَيَكْشِفُ مَا تَدْعُونَ إِلَيْهِ إِن شَآءَ وَتَنسَوْنَ مَا تُشْرِكُونَ

Maana

Bali Yeye ndiye mtakayemuomba, naye atawaondolea mnachomwomba akipenda. Na mtasahau hao mnaowafanya washirika wake.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Bali Yeye ndiye mtakaye mwomba, naye atakuondoleeni mnacho mwombea akipenda. Na mtasahau hao mnao wafanya washirika wake. [41]

[41] Bali nyinyi mnamuelekea Yeye mnapo muomba akakuondoleeni mnacho taka kiondolewe, pindi akipenda. Na mnapo kuwa katika hali hii ya shida mnawasahau hao mnao wafanya ni washirika wake Mwenyezi Mungu!!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Bali hapo mtamuomba Mola wenu Aliyewaumba, si mwingine, na mtamtaka Awaokoe na Awaondolee shida kubwa zilizowashukia Akitaka, kwani Yeye Ndiye Muweza wa kila kitu; na wakati huo mtaacha masanamu wenu na wategemewa wenu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net