Al-An'aam 6:40
الأنعامقُلْ أَرَءَيْتَكُمْ إِنْ أَتَىٰكُمْ عَذَابُ ٱللَّهِ أَوْ أَتَتْكُمُ ٱلسَّاعَةُ أَغَيْرَ ٱللَّهِ تَدْعُونَ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ
Sema: Mwaonaje ikiwajia adhabu ya Mwenyezi Mungu, au ikawajia hiyo Saa, asiyekuwa Mwenyezi Mungu ndiye mtakayemuomba, ikiwa nyinyi ni wakweli?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Mwaonaje ikikujieni adhabu ya Mwenyezi Mungu, au ikakufikieni hiyo Saa - mtamwomba asiye kuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi ni wakweli? [40]
[40] Ewe Nabii! Waambie hawa makafiri: Nambieni, ikikujieni adhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu hapa duniani, au ikikujieni Kiyama kwa vitisho vyake, mtamuelekea yeyote asiye kuwa Mwenyezi Mungu mkimnyenyekea wakati huo akufaeni kwa lolote, kama nyinyi mnasema kweli katika kumuabudu kwenu asiye kuwa Mwenyezi Mungu?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina, «Nipeni habari, ikiwajia adhabu ya Allah Mtukufu ulimwenguni, au ikawajia saa ya nyinyi kufufuliwa, je, mtamuomba hapo asiyekuwa Allah Mtukufu awaondolee shida iliyowakumba, iwapo nyinyi ni wakweli kwamba waungu wenu mnaowaabudu badala ya Allah Mtukufu wanawanufaisha au kuwadhuru?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net