Al-An'aam 6:39
الأنعاموَٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا صُمٌّ وَبُكْمٌ فِى ٱلظُّلُمَـٰتِ ۗ مَن يَشَإِ ٱللَّهُ يُضْلِلْهُ وَمَن يَشَأْ يَجْعَلْهُ عَلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ
Na wale waliozikadhibisha Ishara zetu ni viziwi na mabubu wamo katika giza mbalimbali. Yule ambaye Mwenyezi Mungu anataka, anampoteza, na yule ambaye anataka, anamuweka katika Njia iliyonyooka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na walio kanusha Ishara zetu ni viziwi na mabubu waliomo gizani. Mwenyezi Mungu humwachia kupotea amtakaye, na humweka katika Njia iliyo nyooka amtakaye. [39]
[39] Na ambao hawakuzisadiki dalili zetu zinazo onyesha uwezo wetu na ukweli wa Utume wako, basi hao hawakunafiika na hisiya zao kuwawezesha kuitambua Haki. Kwa hivyo wakawa wanababaika katika upotovu wa ushirikina na inda, kama anavyo babaika kiziwi-bubu katika giza la usiku, hawezi kuepuka kuangamia. Lau kuwa watu hawa wameelekea kheri Mwenyezi Mungu angeli wawezesha wamfikie, kwani Yeye Subhanahu akitaka kumpoteza mtu kwa ufisadi wake alio ukusudia, basi humwachilia mbali na shani yake; na akitaka kumwongoa mtu kwa kuwa makusudio yake ni sawa, basi humsahilishia njia ya Imani iliyo wazi na iliyo nyooka.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wale waliozikanusha hoja za Allah Mtukufu, Aliyetukuka, ni viziwi hawasikii yanayowafaa, ni mabubu hawaitamki haki. Wao wametunduwaa kwenye giza, hawakufuata njia iliyolingana sawa. Yule ambaye Allah Mtukufu Anataka kumpoteza Anampoteza na yule Anayetaka kumuongoza Anamfanya awe kwenye njia iliyolingana sawa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net