Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 38

Al-An'aam 6:38

الأنعام

وَمَا مِن دَآبَّةٍ فِى ٱلْأَرْضِ وَلَا طَـٰٓئِرٍ يَطِيرُ بِجَنَاحَيْهِ إِلَّآ أُمَمٌ أَمْثَالُكُم ۚ مَّا فَرَّطْنَا فِى ٱلْكِتَـٰبِ مِن شَىْءٍ ۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِمْ يُحْشَرُونَ

Maana

Na hakuna mnyama yeyote katika ardhi, wala ndege anayepaa kwa mbawa zake mbili, isipokuwa ni umma kama nyinyi. Hatukupuuza kitu chochote katika Kitabu. Kisha kwa Mola wao Mlezi watakusanywa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hapana mnyama katika ardhi, wala ndege anaye ruka kwa mbawa zake mbili, ila ni umma kama nyinyi. Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote. Kisha kwa Mola wao Mlezi watakusanywa. [38]

[38] Na dalili yenye nguvu kabisa ya uwezo wa Mwenyezi Mungu na hikima yake, na rehema yake, ni kuwa Yeye kaumba kila kitu, na wala hapana juu ya ardhi mnyama anaye tambaa juu yake au chini yake, wala ndege arukaye kwa mbawa zake katika anga, ila Mwenyezi Mungu amewaumba kuwa ni jamii za umati kama mlivyo nyinyi. Na amewajaalia wawe na sifa zao, na vitambulisho vyao, na mipango yao ya maisha yao. Hatukukiacha kitu katika Kitabu kilicho andikwa kilioko kwetu ila tumekithibitisha. Na ikiwa wanakanusha, basi watafufuliwa pamoja na kaumu zote kwa ajili ya hisabu Siku ya Kiyama.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakuna katika ardhi mnyama yoyote anayetembea chini au ndege anayepaa juu kwa mbawa zake isipokuwa ni aina ya makundi yaliyoumbwa kama nyinyi. Hatukuacha katika Allawh, Almaḥfûḍh (Ubao Uliohifadhiwa) chochote isiopokuwa tumekithibitisha. Kisha wao, Siku ya Kiyama, watafufuliwa wapelekwe kwa Mola wao, na hapo Allah Mtukufu Atamhesabu kila mtu kwa alilolitenda.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net