Al-An'aam 6:37
الأنعاموَقَالُوا۟ لَوْلَا نُزِّلَ عَلَيْهِ ءَايَةٌ مِّن رَّبِّهِۦ ۚ قُلْ إِنَّ ٱللَّهَ قَادِرٌ عَلَىٰٓ أَن يُنَزِّلَ ءَايَةً وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ
Na walisema: Kwa nini hakuteremshiwa muujiza kutoka kwa Mola wake Mlezi? Sema: Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuteremsha muujiza. Lakini wengi wao hawajui.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wamesema kwanini hakuteremshiwa Miujiza kutoka kwa Mola wake Mlezi ? Sema: Hakika Mwenyezi Mungu ni muweza wa kuteremsha Miujiza lakini wengi wao hawajui [37]
[37] Na makafiri washupavu wamesema: Tunataka ateremshiwe Muhammad dalili ya kuonekana kutoka kwa Mola wake Mlezi, itayo shuhudia ukweli wa huu wito wake! Waambie, ewe Nabii: Hakika Mwenyezi Mungu anaweza kuteremsha hiyo dalili muitakayo. Lakini wengi wao hawajui nini hikima ya Mwenyezi Mungu katika kuziteremsha Ishara. Na hayo hayafuati matamanio yao. Na lau kuwa Yeye akiwakubalia hilo walitakalo, na kisha wakakanusha baada yake, basi atawateketeza tu. Lakini wengi wao hawajui nini matokeo ya vitendo vyao!!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na washirikina walisema, kwa ujeuri na kiburi, «Kwa nini Allah Mtukufu Hateremshi alama iyoneshayo ukweli wa Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie,) miongoni mwa alama za kimiujiza.» Waambie, ewe Mtume, «Allah Mtukufu ni muweza wa kuwateremshia miujiza, lakini wengi wao hawajui kwamba kuteremsha miujiza kunakuwa kulingana na hekima Yake, Aliyetukuka».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net