Al-An'aam 6:36
الأنعامإِنَّمَا يَسْتَجِيبُ ٱلَّذِينَ يَسْمَعُونَ ۘ وَٱلْمَوْتَىٰ يَبْعَثُهُمُ ٱللَّهُ ثُمَّ إِلَيْهِ يُرْجَعُونَ
Hakika wanaoitikia ni wale wanaosikia. Na ama wafu, Mwenyezi Mungu atawafufua, kisha kwake Yeye ndiko watakakorejeshwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika wanao kubali ni wale wanao sikia. Na ama wafu Mwenyezi Mungu atawafufua, na kisha kwake Yeye ndio watarejeshwa. [36]
[36] Hakika wanao itikia wito wa Haki ni wale wanao ukubali - wale ambao wanao sikia kwa msikio wa kufahamu na kuzingatia. Ama hao walio potoka kabisa hawanafiiki kwa wito wako, kwani wao wamo katika hukumu ya maiti. Na Mwenyezi Mungu atawafufua kutoka makaburini Siku ya Kiyama, na atawarejeza kwake awahisabu kwa waliyo yafanya.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika wale wanaokukubali wewe, ewe Mtume, kwa yale unayoyalingania ya uongofu ni wale ambao wanayasikia maneno kwa kuyakubali. Ama makafiri, wao wamo kwenye hesabu ya wafu. Kwani uhai wa kikweli unakuwa kwa Uislamu. Na wafu, Allah Mtukufu Atawatoa kutoka kwenye makaburi yao wakiwa hai. Kisha watarudi Kwake Siku ya Kiyama ili watimiziwe hesabu yao na malipo yao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net