Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 35

Al-An'aam 6:35

الأنعام

وَإِن كَانَ كَبُرَ عَلَيْكَ إِعْرَاضُهُمْ فَإِنِ ٱسْتَطَعْتَ أَن تَبْتَغِىَ نَفَقًا فِى ٱلْأَرْضِ أَوْ سُلَّمًا فِى ٱلسَّمَآءِ فَتَأْتِيَهُم بِـَٔايَةٍ ۚ وَلَوْ شَآءَ ٱللَّهُ لَجَمَعَهُمْ عَلَى ٱلْهُدَىٰ ۚ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلْجَـٰهِلِينَ

Maana

Na ikiwa ni makubwa kwako huku kupeana kwao mgongo, basi kama unaweza kutafuta njia ya chini kwa chini ya ardhi, au ngazi ya kwendea mbinguni ili uwaletee Ishara. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angelipenda, angeliwakusanya kwenye uongofu. Basi kamwe usiwe miongoni mwa wajinga.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ikiwa ni makubwa kwako huku kukataa kwao, basi kama unaweza kutafuta njia ya chini kwa chini ya ardhi, au ngazi kwendea mbinguni ili uwaletee Ishara -- Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angependa angeli wakusanya kwenye uwongofu. Basi usiwe miongoni mwa wasio jua. [35]

[35] Ikiwa unaona dhiki kwa kukataa kwao kuitikia wito wako, basi kama unaweza kutafuta njia ya kupita chini ya ardhi, au ngazi ya kupandia mbinguni ukawaletea dalili ya kuthibitisha ukweli wako, fanya hivyo! Lakini huna uwezo huo. Basi poa roho yako, na usubiri kungojea hukumu ya Mola Mlezi wako. Lau kuwa Mwenyezi Mungu ange penda basi angeli walazimisha wote hao wayaamini ulio kuja nayo, wakitaka wasitake. Lakini Yeye amewaacha kwa ajili ya kuwafanyia mtihani, kuwajaribu. Basi usiwe miongoni mwa wasio ijua hukumu ya Mwenyezi Mungu na mwendo wake kwa viumbe.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na iwapo umekuwa ni mzito kwako, ewe Muhammad, upinzani wa hawa washirikina na kujiepusha kwao kukubali ulinganizi wako, basi ukiweza kujifanyia mapito ndani ya ardhi, au ngazi ya kupandia mbinguni ili uwaletee alama na dalili ya usahihi wa maneno yako, zisizokuwa hizi tulizokuletea, fanya hivyo. Na lau Allah Mtukufu angetaka kuwakusanya kwenye uongofu ambao nyinyi mnao na kuwaongoza kwenye Imani, Angalifanya hivyo. Lakini Hakulitaka hilo, kwa hekima Anayoijua Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake. Basi, usiwe kabisa ni miongoni mwa wale wajinga ambao huzuni zao zilizidi na wakawa na majonzi mpaka hayo yakawapelekea kwenye babaiko kubwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net