Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 32

Al-An'aam 6:32

الأنعام

وَمَا ٱلْحَيَوٰةُ ٱلدُّنْيَآ إِلَّا لَعِبٌ وَلَهْوٌ ۖ وَلَلدَّارُ ٱلْـَٔاخِرَةُ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ

Maana

Na maisha ya dunia si chochote isipokuwa ni mchezo na pumbao tu. Na hakika Nyumba ya Akhera ni bora zaidi kwa wale wanaomcha Mwenyezi Mungu. Basi, je, hamtumii akili?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na maisha ya dunia si chochte ila ni mchezo na pumbao tu. Na hakika nyumba ya Akhera ni bora zaidi kwa wanao mcha Mungu. Basi, je, hamtii akilini? [32]

[32] Na huo uhai wa duniani walio uona makafiri kuwa ndio uhai wa pekee, na ambao hawaukusudii kwa kufanya vitendo vya kumridhi Mwenyezi Mungu, uhai huo si chochote ila ni mchezo usio kuwa na manufaa, na pumbao la kujipumbazia tu!! Na hakika nyumba ya Akhera ndio khasa uhai wa kweli. Huo unawanufaisha zaidi wale wanao mwogopa Mwenyezi Mungu na wanazifuata amri zake. Basi hamtii akilini jambo hili lilio wazi? Hivyo hamfahamu linalo kudhuruni na linalo kufaeni?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Maisha ya kilimwengu hayakuwa, katika wingi wa hali zake, isipokuwa ni udanganyifu na ubatilifu. Na matendo mema, kwa kutengeneza nyumba ya Akhera, ndiyo bora kwa wenye kumcha Allah Mtukufu, wakajikinga na adhabu Yake kwa kumtii na kujiepusha na mambo ya kumuasi. Kwani hamuelewi, enyi washirikina mlioghurika na pambo la uhai wa kilimwengu, mkayatanguliza yanayosalia mbele ya yanayomalizika?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net