Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 33

Al-An'aam 6:33

الأنعام

قَدْ نَعْلَمُ إِنَّهُۥ لَيَحْزُنُكَ ٱلَّذِى يَقُولُونَ ۖ فَإِنَّهُمْ لَا يُكَذِّبُونَكَ وَلَـٰكِنَّ ٱلظَّـٰلِمِينَ بِـَٔايَـٰتِ ٱللَّهِ يَجْحَدُونَ

Maana

Hakika tunajua ya kwamba yanakuhuzunisha yale wanayoyasema. Basi hakika wao hawakukadhibishi wewe, lakini hao madhalimu wanazikataa Ishara za Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Tunajua ya kwamba yanakuhuzunisha wanayo yasema. Basi hakika wao hawakukanushi wewe, lakini hao madhaalimu wanazikataa Ishara za Mwenyezi Mungu. [33]

[33] Ewe Nabii! Sisi tunajua kuwa yanakuhuzunisha haya wayasemayo makafiri ili kukukadhibisha. Basi wewe usihuzunike kwa hayo. Kwani hakika wao hawakutuhumu wewe kuwa ni mwongo, walakini wao kwa kujidhulumu nafsi zao na kuidhulumu haki, wanashindana kwa inda, na wanazikanya kwa ndimi zao dalili za ukweli wako, na alama za Unabii wako.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika sisi tunajua kwamba msimamo wa kaumu zako wa kukukanusha waziwazi unakutia huzuni moyoni mwako. Basi subiri na ujitulize. Kwani wao hawakukanushi wewe kutoka ndani ya roho zao; wao waamini ukweli wako, lakini wao kwa udhalimu na uadui walionao, wanazikataa hoja zilizo wazi zinazoonyesha ukweli wako, ndipo wakakufanya mrongo kwa yale uliyokuja nayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net