Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 31

Al-An'aam 6:31

الأنعام

قَدْ خَسِرَ ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِلِقَآءِ ٱللَّهِ ۖ حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَتْهُمُ ٱلسَّاعَةُ بَغْتَةً قَالُوا۟ يَـٰحَسْرَتَنَا عَلَىٰ مَا فَرَّطْنَا فِيهَا وَهُمْ يَحْمِلُونَ أَوْزَارَهُمْ عَلَىٰ ظُهُورِهِمْ ۚ أَلَا سَآءَ مَا يَزِرُونَ

Maana

Hakika wamehasirika wale waliokadhibisha kukutana na Mwenyezi Mungu, mpaka ilipowajia Saa kwa ghafla, wakasema: 'Ee majuto yetu kwa yale tuliyoyapuuza!' Nao watabeba mizigo yao juu ya migongo yao. Tazama! Ni maovu mno hayo wanayoyabeba.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika wamekhasirika walio kanusha kukutana na Mwenyezi Mungu, mpaka ilipo wajia Saa kwa ghafla, wakasema: Ole wetu kwa tuliyo yapuuza! Nao watabeba mizigo yao juu ya migongo yao. Ni maovu hayo wanayo yabeba. [31]

[31] Hakika wamekhasiri walio kanya kukutana na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya hisabu na malipo ya Siku ya Kiyama, na wakaendelea na kukanusha kwao mpaka yalipo wafuma mambo ya Siku ya Kiyama wakajuta na wakasema: Ole wetu (yaani msiba wetu) kwa kupuuza kwetu kuifuata Haki huko duniani! Nao siku hiyo watakuwa wanaanguka kwa kuemewa na uzito wa dhambi zao! Ni mabaya mno hayo madhambi wanayo yabeba!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wamepata hasara wale waliokanusha kufufuliwa baada ya kufa. Mpaka Kiyama kitakaposimama na wakashtushwa kwa mwisho mbaya, watazipigia nafsi zao kelele za majuto juu ya kile walichokipoteza katika maisha yao ya ulimwenguni, hali ya kwamba wanabeba madhambi yao juu ya migongo yao. Ni mibaya iliyoje mizigo hiyo mizito iliyo miovu ambayo wataibeba!

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net