Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 30

Al-An'aam 6:30

الأنعام

وَلَوْ تَرَىٰٓ إِذْ وُقِفُوا۟ عَلَىٰ رَبِّهِمْ ۚ قَالَ أَلَيْسَ هَـٰذَا بِٱلْحَقِّ ۚ قَالُوا۟ بَلَىٰ وَرَبِّنَا ۚ قَالَ فَذُوقُوا۟ ٱلْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ

Maana

Na lau utaona walivyosimamishwa mbele ya Mola wao Mlezi, akasema, "Je, huu si uhakika?" Na wao wakasema, "Ndiyo? Tunaapa kwa Mola wetu Mlezi (ni uhakika)." Yeye akasema: Basi onjeni adhabu kwa sababu ya vile mlivyokuwa mnakufuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na lau ungeli ona watavyo simamishwa mbele ya Mola wao Mlezi, akawaambia: Je, si kweli haya? Na wao watasema: Kwani? Tunaapa kwa Mola Mlezi wetu ni kweli. Yeye atasema: Basi onjeni adhabu kwa sababu ya vile mlivyo kuwa mnakataa. [30]

[30] Lau ungeli waona watavyo simama mbele ya Mola wao Mlezi kwa ajili ya kuhisabiwa, na wao wanaujua ukweli wa aliyo wateremshia Mwenyezi Mungu Mitume wake, ungeli ona uovu wa hali yao pale Mwenyezi Mungu atapo waambia: Je, haya mnayo yashuhudia sasa sio kweli mliyo kuwa mkiikataa huko duniani kwenu? Nao watajibu hali ni wanyonge: Kwani! Tunaapa kwa Mola Mlezi wetu, ni kweli! Tena baada ya hayo Mwenyezi Mungu atawaambia: Ingieni Motoni kwa sababu ya mlivyo kuwa mmeshikilia ukafiri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau utawaona, ewe Mtume, wenye kukanusha kufufuliwa watakapofungwa mbele ya Allah Mtukufu, Aliyetukuka, ili uamuzi wa Allah Mtukufu upite kuhusu wao Siku ya Kiyama, ungaliona hali mbaya sana, pindi Allah Mtukufu, Aliyetukuka na kuwa juu, Atakaposema, «Je, ufufuzi huu, mliokuwa mkiukanusha ulimwenguni, si kweli?» Watasema, «Kwani? Tunaapa kwa Mola wetu kuwa huu ni kweli.» Hapo Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Atasema, «Basi onjeni adhabu kwa mlivyokuwa mkikufuru,» yaani, adhabu ambayo mlikuwa mkiikanusha ulimwenguni kwa sababu ya kumkataa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na Mtume Wake Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net