Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 29

Al-An'aam 6:29

الأنعام

وَقَالُوٓا۟ إِنْ هِىَ إِلَّا حَيَاتُنَا ٱلدُّنْيَا وَمَا نَحْنُ بِمَبْعُوثِينَ

Maana

Na walisema: Hakuna mengine isipokuwa maisha yetu haya ya duniani, wala sisi hatutafufuliwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na walisema: Hakuna mengine ila maisha yetu haya ya duniani, wala sisi hatutafufuliwa. [29]

[29] Na lau wakirejeshwa duniani watairudia ile ile sera yao ya mwanzo, na watasema: Hatuna sisi uhai mwingine ila huu huu uhai wa kidunia. Wala sisi hatutafufuliwa baadae.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hawa washirikina wanaokanusha kufufuliwa wanasema, «Hakuna maisha isipokuwa maisha haya tuliyonayo, na sisi si wenye kufufuliwa baada yakufa kwetu».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net